Rais Magufuli alisema
:
“Watumishi wa serikali lazima watoe tija na ndiyo maana Marehemu alikuwa mkali kutaka kuona matokeo ya kinachofanywa, kwa hiyo kile na mimi kilinipa mafunzo pia,”
habarileo Thursday, May 5, 2022 12:03:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Mambo ni mengi, sidhani kama kuna fundi anaweza kusema mimi fundi kwenye nafasi ya urais, sijui au labda mimi kwa sababu ya ugeni, mwaka mmoja, lakini sidhani kama unazoeleka,”
habarileo Thursday, May 5, 2022 12:03:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
(
about Rais Magufuli
)
:
“Mshituko lazima, mshituko haukuwa kubeba yale majukumu, mshituko ulikuwa kwenye lililotokea lililonifanya nibebe yale majukumu, lakini kwa kazi zilizokuwepo, si mshituko mkubwa kwa sababu si nilikuwa Makamu wa Rais na nilikuwa namsaidia kwa karibu Mheshimiwa Rais, kwa hiyo kazi nilikuwa nazifahamu,”
habarileo Thursday, May 5, 2022 12:03:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Miradi hii yote ikikamilika, kero ya msongamano wa magari jijini Dar es Salaam itapungua kwa kiasi kikubwa sana na hii itakuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa shughuli za kiuchumi na biashara,”
habarileo Friday, March 25, 2022 11:13:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kwa ujumla Mzee Magufuli alikuwa akitamani kuiona Tanzania iliyojikomboa na kujitegemea kiuchumi. Nikasema na mimi nitaliongoza taifa katika mwelekeo huohuo,”
habarileo Friday, March 18, 2022 9:18:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Narejea wito wangu, kuomba tuendelee kuelimishana na kuhamasisha kushiriki katika utaratibu wa kuweka anuani ya makazi na baadaye kushiriki kwenye sensa itakayofanyika Agosti mwaka huu,”
habarileo Friday, March 18, 2022 9:18:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Lakini leo hii tunashiriki kama wabia muhimu wa uchimbaji wa rasilimali zetu hizi muhimu na adhimu ambazo zina nafasi ya kipekee katika kuiletea nchi yetu maendeleo ya uchumi. Hatuna budi kujipongeza kwa hatua hii kubwa tuliyofikia,”
habarileo Tuesday, December 14, 2021 11:02:00 AM EAT
Rais Magufuli alisisitiza
:
“niwaombe tu wizara kwa sababu mmeshakubaliana jana usiku na ratiba ilikuwa imeshatengenezwa, nakupeni uwezo mkitoka hapa mwende mkasaini nao na kazi ianze mara moja,”
habarileo Tuesday, December 14, 2021 11:02:00 AM EAT
Rais Magufuli alisisitiza
:
“Wazee wangu mtashuhudia mabadiliko ambayo nia yake ni kutengeneza na si kubomoa, mkiona tunaleta mabadiliko mjue tuna nia njema ya kujenga nchi na si kubomoa, katika mabadiliko haya kijana wako akiguswa basi mjue ni kwa nia njema tunataka tuipeleke Tanzania juu zaidi,”
habarileo Saturday, May 8, 2021 7:52:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
(
about John Magufuli
)
:
“Naomba kutumia jukwaa hili la Bunge kusema mambo mawili. Kwanza ni kuwaonya wale wote wanaodhani kuwa usimamizi wa mali za umma, kusimamia ukwepaji wa kodi, kusimamia uzibaji wa mianya ya kupoteza mapato, kukemea uzembe na wizi, yameondoshwa kutokana na kuondoka kwa Mheshimiwa Hayati Dk John Magufuli,”
habarileo Wednesday, April 28, 2021 2:37:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Ukiingia kwenye mitandao ya kijamii kuna uzandiki mkubwa sana. Kila mtu anazua lake. Kila analofikiri kichwani kwake anaweka kule na kuwaaminisha watu wananchi mambo kadhaa, kadhaa, kadhaa”
habarileo Monday, April 19, 2021 7:24:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
"Inasikitisha kuona wanapiga ngoma mitandaoni na kuchezwa bungeni kwa kudemka vizuri. Kulinganisha watu wala si kulinganisha agenda za kitaifa"
habarileo Monday, April 19, 2021 7:24:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
"Yaani kwenye eneo lote kuanzia Tanga hadi Mtwara kusijengwe bandari yoyote. Bandari ya Kilwa tusiiendeleze, Bandari ya Mtwara ambayo itawezesha mikoa ya Kusini kupokea mafuta badala ya Dar es Salaam kisha yarudihuko, hatutakiwi kuiendeleza, barabara kutoka Mtwara hadi Bamba Bay ambayo itatuwezesha kusafirisha mizigo hadi Msumbiji tusiijenge,"
bbc-swahili Wednesday, April 14, 2021 2:20:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Unapochelewesha malipo ili yatengeneze riba kwa serikali, sikuelewi na ni kuongeza gharama za miradi lakini pia ni ucheleweshaji wa kazi kwa mkandarasi,”
habarileo Tuesday, April 6, 2021 5:41:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kasimamieni miradi iendelee lakini kuwe na displine (nidhamu) ya fedha. Fedha za maendeleo zitengwe na ziende kunakohusika kwa utaratibu. Kuna fedha zinaombwa za miradi haziji....kasimamieni hayo,”
habarileo Tuesday, April 6, 2021 5:41:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kwa ajili ya kumuenzi, naomba kamilisheni tuone jinsi tunaweza kufanya,”
habarileo Saturday, March 27, 2021 4:52:00 AM EAT
Rais Magufuli amesisitiza
:
“Wakati wa kampeni zetu tulitoa ahadi za kukamilisha upatikanaji wa maji Tanzania. Katika miaka mitano iliyopita tumeweza kutekeleza upatikanaji wa maji kwa Watanzania kwa asilimia 75, tumebakiwa na asilimia ndogo ambayo tunakwenda kuimalizia ndani ya miaka mitano hii, nawahakikishia Watanzania tunakwenda kumalizia palipobakia,”
habarileo Friday, March 26, 2021 8:34:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Leo si siku nzuri ya kwangu kusema, kutokana na kidonda kikubwa moyoni na mzigo mzito nilio nao. Nimekula kiapo katika mazingira tofauti, nimezoea kula kiapo katika hali ya nderemo na furaha, lakini leo nimekula kiapo katika hali ya huzuni na masikitiko,”
habarileo Wednesday, March 24, 2021 7:54:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Mimi nimeandaliwa vizuri nitaendeleza pale aliopoishia na kukamilisha na tutahakikisha tunafanikisha na kufika Tanzania mahali alipotaka Tanzania ifike,”
habarileo Tuesday, March 23, 2021 8:01:00 AM EAT
Rais Magufuli alieleza
:
“Afrika tumepoteza mwanasiasa mkongwe aliyelenga kutetea na kulinda mali za Afrika na watu wake. Tutabaki na kumbukumbu mpiganaji wetu na mzalendo wa kweli, sio tu kwa maslahi mapana ya Watanzania, bali ya Umoja wa Afrika, mtetezi wa uhuru na Bara la Afrika aliyelenga kutimiza ndoto za mshikamano za waasisi wetu wa Bara la Afrika,”
habarileo Tuesday, March 23, 2021 3:16:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Pia namshukuru kwa juhudi zake za kuelekea ukombozi na mafanikio ya kiuchumi kwa nchi yake, kikanda na bara zima, alikuwa Kiongozi aliyetaka masuala ya tamaduni, mila na desturi yatumike kutatua changamoto mbalimbali zilizopo,”
habarileo Monday, March 22, 2021 6:33:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
"Kwa wale ambao wana mashaka mwanamke huyu ataweza kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nataka niwambie huyu aliyesimama hapa ni rais, wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye maumbile yake ni mwanamke,"
deutschewelle-sw Monday, March 22, 2021 6:25:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Waliposema miradi mikubwa ya miundombinu haiwezi kukamilishwa kwa wakati, walimwona Magufuli akifanya. Kila mmoja ameona na hakutaka kufuata maelekezo ya taasisi za kifedha ambazo zimekuwa zikiacha Afrika na madeni makubwa,”
habarileo Monday, March 22, 2021 3:21:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Afrika tumepoteza mwanasiasa mkongwe aliyelenbga kutetea na kulinda mali za Afrika na watu wake,”
habarileo Monday, March 22, 2021 2:33:00 PM EAT
Rais Magufuli alieleza
:
“Niwahakikishie kuwa tupo imara kama taifa, na sisi viongozi wenu tumejipanga vizuri kuhakikisha tunaendelea pale mwenzetu alipoishia,”
habarileo Saturday, March 20, 2021 7:53:00 AM EAT
Rais Magufuli alieleza
:
“Niwahakikishie kuwa tupo imara kama taifa, na sisi viongozi wenu tumejipanga vizuri kuhakikisha tunaendelea pale mwenzetu alipoishia,”
habarileo Saturday, March 20, 2021 3:05:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Nakumbuka kwa dhati mara nyingi tulikutana na kuongea kuhusu maendeleo ya nchi zetu mbili, nakumbuka safari yake rasmi ambayo alitutembelea hapa Kenya na kwa pamoja tukafungua barabara ambayo tunaiita Southern by Pass,”
habarileo Friday, March 19, 2021 10:17:00 AM EAT
Rais Magufuli aliongeza
(
about Afrika Mashariki
)
:
“Mimi pia alinialika nimtembelee kule kwake Chato na nikapata nafasi ya kumsalimia mama yake na kuongea naye. Nililala nyumbani kwake na tukaongea mengi kuhusu nchi zetu mbili na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla,”
habarileo Friday, March 19, 2021 10:17:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Natoa salamu zangu za rambirambi kwa familia yake na watu wa Tanzania ambao tunatumia wote mpaka na urithi wetu,”
habarileo Friday, March 19, 2021 10:17:00 AM EAT
Rais Magufuli Alisema
:
“Unakuja mtaani unafanya biashara unapeleka chakula nyumbani; maisha yanakwenda”
habarileo Friday, March 19, 2021 6:21:00 AM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Kwa niaba ya serikali na watu wa Kenya natuma salamu za pole na rambirambi kwa mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, watoto na familia yote ya Magufuli na Watanzania, nakumbuka mara nyingi ambapo tumeweza kukutana na kuongea maendeleo ya nchi zetu, nimepoteza rafiki, mfanyakazi mwenzangu na mshirika wangu, Kenya tunasimama imara wakati huu mgumu na Watanzania,”
mtanzania Thursday, March 18, 2021 7:12:00 PM EAT
Rais Magufuli anasema
:
"Nipende kuwaambia wanawake kuwa serikali yangu itaendelea kuwaamini na kuwapa nafasi mbalimbali za kiuongozi wanawake maana nimeona ni jinsi gani mnachapa kazi na ndio maana hata Makamu wa Rais (Samia Suluhu) ni mwanamke na pia, nikupongeze na wewe Dk Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuendelea kuwa Naibu Spika,"
habarileo Wednesday, March 10, 2021 6:54:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Hatuna tena muhali na wahalifu wanaotumia silaha wala kujihusisha na ugaidi, Watanzania walishasahahu kunyang’anywa fedha zao, sasa tunasema mama mkanye mwanao, mke mtunze mumeo, vinginevyo mtawakosa. ”
habarileo Saturday, February 27, 2021 11:12:00 AM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Watendaji wa Serikali wawe wepesi kutoa taarifa sahihi kwa waandishi wa habari, utakuta yamefanyika mambo mazuri lakini hayatolewe na wananchi hawayafahamu, tusiogope kukosolewa, lakini vyombo vya habari toeni taarifa za ukweli bila kuweka chumvi, zingatieni ukweli,”
mtanzania Saturday, February 27, 2021 10:18:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Vyombo vya habari mnajitahidi kutoa habari, lakini mtangulize sana uzalendo na hakikwa yule anayeandikiwa habari, kumekuwepo na uzushi sana mara fulani kafa ni mambo ya ajabu,”
mtanzania Saturday, February 27, 2021 10:18:00 AM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Muheshimiwa IGP umezungumza kuhusu hao wafungwa wa uhalifu mbalimbali wa kutumia silaha ambao wakifungwa wakirudi wanaendelea kurudia matukio hawataki kuyaacha, kama alikuwa jambazi anaendelea na ujambazi muwalazimishe sasa wayaache kwa nguvu na hilo najua halitakushindwa IGP”
habarileo Friday, February 26, 2021 3:47:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Kutopata mafao ni tatizo la wakubwa wenu wizarani kama mpo hapa wastaafu mumlaumu Waziri mwenye dhamana na watendaji wake huo ndio ukweli wakitaka wastaafu kulipwa watalipwa tena haiwezi kuchukua hata siku tano kama watakuwa na mawasiliano mazuri na Wizara ya Fedha,”
habarileo Friday, February 26, 2021 2:57:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
"Manispaa ya Ilala mnastahili, hamkupendelewa, ni haki yenu kwa sababu hata katika mapato mnaongoza. Kwa nini mlinganishwe na manispaa nyingine, na kwa uamuzi huo aliyekuwa Meya wa Ilala ndiye Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na Naibu Meya wake"
habarileo Friday, February 26, 2021 7:01:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
"Nyie ndio mabosi wa jiji hili (Dar es Salaam) na nyie ndio mabosi wangu nitakapokuwa nakuja jijini humo, na madiwani wa Manispaaa ya Ilala ndio madiwani wa jiji na bajeti yenu itaongezeka na kuwa kubwa ili itumike kusaidia kutatua changamoto za jiji na maeneo yake yote,"
habarileo Friday, February 26, 2021 7:01:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kwa hiyo tujiandae kisaikolojia wale waliokuwa wanautaka umeya wa jiji la Dar, Meya atapatikana kutoka Ilala au mojawapo ya Manispaa za hapa,draft (rasimu) ya kubadilisha jiji hili nimeshaletewa na Jaffo nikitoka hapa nakwenda kuisaini ili turahisishe mambo, tuokoe fedha zilizokuwa zinapotea”
habarileo Thursday, February 25, 2021 9:44:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Tumepata alama ya pekee ya jiji hili, tuitunze idumu miaka mingi, barabara hizi zinasaidia kuondoa msongamano wa magari kwenye makutano haya, kwa maana sasa unapita moja kwa moja kwenda ama Mwenge, au Kimara, au Buguruni au Posta hakuna tena msongamano,”
habarileo Thursday, February 25, 2021 9:44:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Wabunge na watendaji wote lazima tuwe tunatembelea maeneo yetu na sio kusubiri kuona taarifa mitandaoni, kama ile Shule ya King’ongo, tujipange kutatua kero, nashukuru RC (Mkuu wa Mkoa) wa Dar es Salaam alivamia pale na kuanza kushughulikia, lakini kwa kweli ile shule ingekuwa hadi leo haijajengwa mngekoma, nilitaka kutoa demo, nigeanzia na RC, DC (Mkuu wa Wilaya), Mkurugenzi, sijui Mwenyekiti wa council (baraza) mpaka mwenyekiti wa Kijiji na Waziri”
habarileo Thursday, February 25, 2021 9:44:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Tunawajibu wa kuwatumikia wananchi huo ndio mkataba wetu kwao, kwa hiyo RC nakushukuru malaika walikugusa ukawahi haraka haraka, nilikuwa nakuangalia, nikasema una bahati kwa sababu mkuu wako wa wilaya alishaanza kulalamika akasema wanatumiwa, sasa wanatumiwa wakati wanaeleza ukweli, kwa hiyo sisi tunawajibu wa kutekeleza yale tunayotakiwa kutekeleza”
habarileo Thursday, February 25, 2021 9:44:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kijazi alikuwa hakai ofisini, alikuwa anatembelea barabara zake. Mwaka 2000 baada ya uchaguzi, nikachaguliwa kuwa Waziri, nilipokuwa Waziri nikajua Rais Mkapa ataniletea Katibu Mkuu mwingine, siyo kawaida kwa waziri kuomba Katibu Mkuu, nikaja Ikulu kumuona Mzee Mkapa, kumuomba Balozi Kijazi awe Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,”
habarileo Saturday, February 20, 2021 5:04:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Ikaisha miaka miwili. Mwaka 2019 sikupata. Nikamwongeza tena miaka mingine miwili, kwa hiyo natoa pole sana kwa familia,”
habarileo Saturday, February 20, 2021 5:04:00 AM EAT
Rais Magufuli alisisitiza
:
“Tuendelee ndugu zangu Watanzania kusimama na Mungu, tulishinda mwaka jana, inawezekana hili ni jaribu jingine, nalo tukisimama na Mungu tutashinda, tusitishane na kuogopeshana tutashindwa kufika. Inawezekana kuna mahali tumemkosea Mungu, inawezekana kuna mahali tunapata jaribu kama Waisraeli walivyokuwa wakienda Kaanani. Tusimame na Mungu ndugu zangu Watanzania,”
habarileo Saturday, February 20, 2021 5:04:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Hata sasa hatutaweka ‘lock down’ kwa sababu tunajua Mungu yupo siku zote. Niliona nitoe huu wito ndugu zangu kwa sababu mimi ni kiongozi wenu, nina wajibu wa kuwakumbusha kwamba taifa hili liko mikononi mwa Mungu na Mungu ataendelea kusimama,”
habarileo Saturday, February 20, 2021 5:04:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar Dk Mwinyi, familia, Wazanzibari, wanachama wa ACTWazalendo na Watanzania wote. Mungu amweke mahali pema peponi, Amina,”
habarileo Thursday, February 18, 2021 8:49:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Bidhaa zenu zinaitwa Korie, naomba mwekezaji aangalie kutengeneza jina jingine linalohusu Tanzania kwa sababu Tanzania tunazalisha vitu vingi, kwa mfano maparachichi yanazalishwa Iringa yanawekwa nembo ya nchi zingine, inafaa pawepo na jina linalotangaza Tanzania kwa kuwa itakuwa njia ya kuitangaza nchi yetu. Tuwe na nembo ya Kitanzania ambalo ni jambo muhimu katika kujenga uzalendo, lazima tujivunie uzalendo wetu,”
habarileo Saturday, February 13, 2021 6:18:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Nampongeza mwekezaji kwa kujenga kiwanda hiki kwa kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 20 sawa na zaidi ya Sh bilioni 40. Kiwanda hiki ni kikubwa kuliko vyote nchini na kina uwezo wa kukoboa tani 288 za mpunga kwa siku, kinatoa ajira ya watu 75 za moja kwa moja lakini wanufaika ni wengi,”
habarileo Saturday, February 13, 2021 6:18:00 AM EAT
Rais Magufuli alisisitiza
:
“Wote waliopewa viwanda na hawajaviendeleza tuvichukue, waziri usichelewe wala kutazama sura ya mtu, tena wakati huu ambao mimi nipo ndiyo wa kuyang’anya viwanda hivyo, nikiondoka yatarudi yaleyale,”
habarileo Saturday, February 13, 2021 5:29:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Ndiyo maana leo (jana) nakupongeza sana Rostam kwa uwekezaji huu, kweli nakupongeza kwa sababu ndugu yako Abood mbunge wa hapa ameshindwa kuviendesha viwanda viwili vya Canvas na Moproco. Kiwanda cha Moproco kilikuwa kinazalisha mafuta ya kupikia, lakini mbunge wetu ulipewa hivi viwanda tangu mwaka 1996 mpaka uliponyang’anywa mwaka jana, kwa hiyo ukawanyima ajira wapiga kura wako,”
habarileo Saturday, February 13, 2021 5:29:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Sasa nimeshangaa sana na kweli nimeumia sana, mtu anakuja na kiroba chake cha vitunguu, akifika hapa anamkuta mtu wa manispaa anataka kudai pesa ya kuingiza biashara, anadai pesa ya kizimba na zingine, lakini kitu kingine nilichokiona humu kuna watu waliopewa vizimba vyao bila tatizo, lakini wapo wengine waliopewa vizimba kwa kukodishwa na madalali,”
habarileo Friday, February 12, 2021 4:08:00 AM EAT
Rais Magufuli alisisitiza
(
about Rais Magufuli
)
:
“Sitaki raia wasumbuliwe wakati mimi nikiwa Rais,”
habarileo Friday, February 12, 2021 4:08:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Mheshimiwa Jaji Mkuu Watanzania watakuheshimu kwa historia. Umefanya mambo mengi lakini hili nalo limalizie. Mheshimiwa Jaji Kiongozi na waheshimiwa majaji, ndugu zangu wananchi wanalia kwa hukumu ambazo hawawezi wakazisoma. Kutafsiri tu kwenyewe lazima walipe pesa. Tunatengeneza mateso na machozi kwa wananchi wengi, muwaonee huruma Watanzania”
habarileo Wednesday, February 3, 2021 6:18:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kuna wakati magereza yalikuwa na wafungwa zaidi ya 38,000, hivyo naunga mkono rai ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa waheshimiwa majaji na mahakimu kutoa dhamana na adhabu mbadala kila inapostahili. Hii si tu itapunguza rudikano wa wafungwa na mahabusu kwenye magereza bali pia itaipunguzia serikali mzigo wa kuwahudumia wafungwa.”
habarileo Tuesday, February 2, 2021 9:42:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Nimesikia kwamba kamati za maadili za maofisa wa Mahakama wa mikoa na wilaya ambazo kisheria zinaongozwa na Ma-RC na Ma-DC hazikutani, wamepewa madaraka ili kushughulikia masuala ya maadili hawakutani hivyo kushindwa kuchukua hatua kwa watumishi wenye makosa”
habarileo Tuesday, February 2, 2021 9:42:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Wewe hapa Jaji Mkuu umezungumza tena Kiswahili sanifu kweli kizuri kuliko changu cha Kisukuma lakini ukienda kuhukumu kule unaandika Kingereza, hicho Kiswahili unachokitumia hapa kimepotelea wapi. Hii ni challenge (changamoto) kubwa, ni lazima tubadilike, ni lazima tukipende kilicho chetu”
habarileo Tuesday, February 2, 2021 6:34:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Huyu amekuwa mzalendo wa kwanza kuandika kwa lugha ya Kiswahili. Tunamuenzi Baba wa Taifa kwa kuanzisha Mahakama, kwa kuanzisha chuo kikuu, lakini Baba wa Taifa ndiye aliyeanzisha Kiswahili hukumu zenu mnazitoa kwa Kingerezahuyu ni shujaa wa Kiswahili katika Mahakama. Mnajua na ninyi katika Mahakama mpo very rigid (hamtaki kubadilika)”
habarileo Tuesday, February 2, 2021 6:34:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Huyu ameamua, na kwa sababu ameamua kuenzi lugha ya Kiswahili mimi leo ninampandisha cheo kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa”
habarileo Tuesday, February 2, 2021 6:34:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Wewe hapa Jaji Mkuu umezungumza tena Kiswahili sanifu kweli kizuri kuliko changu cha Kisukuma lakini ukienda kuhukumu kule unaandika Kingereza, hicho Kiswahili unachokitumia hapa kimepotelea wapi. Hii ni challenge (changamoto) kubwa, ni lazima tubadilike, ni lazima tukipende kilicho chetu,”
habarileo Monday, February 1, 2021 4:28:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kahama asilimia 50 ya miradi ya maendeleo inafanywa kwa mapato yao ya ndani na nyie fanyeni kazi, wilaya sio Bahi tu. Halmashauri hii ilikuwa inaliwa sana, Mbunge kasimamie fedha za wananchi nitakuwa nafuatilia, Dodoma na Bahi si mbali nitafuatilia maendeleo,”
habarileo Sunday, January 31, 2021 4:09:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Sheria ya Ardhi Namba 5....hata kama una plot (eneo) lako la makazi na hujaendeleza unanyang’anywa, ila kwa heshima yako mama, naagiza DC na Mkurugenzi wa Halmashauri hii ya Bahi kumpa shamba ekari tatu mama huyu,”
habarileo Sunday, January 31, 2021 1:02:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Lakini mradi huu ni mkubwa, una uwezo wa kutoa maji lita milioni 9.8 kwa siku sawa na asilimia 213.33 ya mahitaji ya miji hiyo miwili na hivyo kuwa na ziada ya asilimia 113 na tumeamua mradi huu uhudumie pia vijiji vingine 22 vyenye watu 63,000”
habarileo Saturday, January 30, 2021 6:34:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Ni imani yangu kuwa miradi hii na mingine mingi ikikamilika, itatoa huduma kwa wananchi na ninataka miradi hiyo itoe maji sitaki miradi ya kichefuchefu wala hewa”
habarileo Saturday, January 30, 2021 6:34:00 AM EAT
Rais Magufuli alisisitiza
:
“Umeanza vizuri hongera sana,moto ulioanza nao endelea nao, usicheke na hawa wakandarasi kamwe, cheka wakati unakunywa maji, halafu zungumzeni na Bodi ya Makandarasi ili kupitia Sheria Namba 17 ya mwaka 1997, wafutwe, wasipate kazi popote Tanzania, kwa vile tuna ushirikiano ndani ya EAC pelekeni majina yao, hatuhitaji watu wa ovyo nchi hii, tunataka ukipewa pesa fanya kazi,”
habarileo Saturday, January 30, 2021 6:34:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Hili nalo tutaliangalia je hawa watumishi wa afya ambao tunaruhusu waajiriwe wanapangwa wapi? Kwa sababu inawezekana tunapanga kuajiri, hawa watumishi wanabaki Dar es Salaam, hawatawanywi kwenye maeneo,”
habarileo Thursday, January 28, 2021 9:11:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Nilijaribu kujiuliza vizuri kama bajeti hiyo imeongezeka kama ilivyoonekana ni sawa na bajeti ya afya nchi nzima ilivyoongezeka kutoka Sh bilioni 31 mwaka 2015 hadi mwaka 2020 ambako ilifikia Sh bilioni 270 sasa inakuaje dawa hazipatikani, kuna mahali kuna tatizo,”
habarileo Thursday, January 28, 2021 9:11:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Unajifukizia huku unamuomba Mungu unaswali, unasali huku unapiga zoezi la kufanya kazi, la kulima mahindi na kulima viazi, ili ule vizuri ushibe corona ishindwe kuingia,”
habarileo Thursday, January 28, 2021 6:04:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Tusisubiri mpaka wakati wa uvunaji ufike ndipo muanze kuhangaika kutafuta mahali pa kupeleka magogo, ni lazima tuachane na utaratibu wa sasa wa kuuza nje magogo. Bahati mbaya kwenye magogo nako tunalaliwa sana,”
habarileo Thursday, January 28, 2021 6:04:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Wenzetu wamefaidika sana na sekta ya mifugo sisi hatujanufaika. Wao wanatengeneza mabegi, mikanda na viatu yenye soko kubwa Ulaya. Nimezungumza na rais na kumuomba kukaribisha wawekezaji lakini pia kuangalia ni namna gani ya kujifunza kwao ili kuendeleza sekta hiyo,”
habarileo Tuesday, January 26, 2021 5:29:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Waasisi wa mataifa yetu Mwalimu Julius Nyerere na hayati Mfalme Haile Sellasie walikuwa mstari wa mbele katika uanzishwaji wa OAU na harakati za ukombozi mwaka 1963. Tumeendelea na ushiano huo mkubwa ulionufaisha nchi zetu katoka nyanja mbalimbali,”
habarileo Tuesday, January 26, 2021 5:29:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Lakini pia Watanzania wamekuwa wakipata fursa ya masomo nchini Ethiopia ambapo jumla ya marubani 75 na wahandisi wa ndege 20 wanasoma Ethiopia,”
habarileo Tuesday, January 26, 2021 5:29:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Uwanja wetu kule Ethiopia tuliochelewa kuujenga kwa sababu hela tulizopeleka kule zililiwa na balozi wetu na kiwanja tukakirudisha kwa kushindwa kutimiza masharti tumemuomba aturudishie na tumemuahidi tutakiendeleza kwa kujenga,”
habarileo Tuesday, January 26, 2021 5:29:00 AM EAT
Rais Magufuli amesisitiza
:
“Wananchi wamechoka na michakato kwa kuwa mradi huo umechelewa kutekelezwa tangu mwaka 1976 mimi wakati huo nikiwa mwanafunzi wa kidato cha pili, hakikisheni utekelezaji wake unaanza haraka na msitishwe na maneno ya watu watakaojitokeza kupinga uwekezaji huu,”
habarileo Tuesday, January 26, 2021 3:08:00 AM EAT
Rais Magufuli amesema
(
about Martha Umbulla
)
:
“Umbulla alikuwa mpole, mchapakazi, na mpenda maendeleo. Nazikumbuka jitihada zake za uongozi akiwa Mkuu wa Wilaya na akiwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”
habarileo Thursday, January 21, 2021 4:21:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Namshukuru Mungu kuona mradi huu kama utaanza mapema, ninaiamini sana timu yangu ya majadiliano ambayo ina wataalamu wa kutosha, nina imani kubwa ni waaminifu na watiifu kwa taifa lao, madini ya nickel yanatumika kutengenezea vitu mbalimbali vikiwemo vifaa vya kielektroniki, kutengenezea vyuma vigumu, bidhaa za kuzuia kutu na hutumika kwenye injini za ndege,”
habarileo Wednesday, January 20, 2021 7:41:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Na Naibu Waziri ukamweleze Waziri mwezako, na ninyi wabunge mkamweleze Waziri kwamba huu mradi nataka uishe. Huyu mkandarasi kama hawezi kufanya kazi fukuzeni, hakuna kubemelezana hapa, hatukuja kubembelezana, hapa ni kazi tu. Contractor (mkandarasi) usipofanya kazi vizuri unaondokanataka maji”
habarileo Tuesday, January 19, 2021 8:02:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
”Kuna shule moja ya msingi Ubungo, Dar Es Salaam inatwa Barango, ina wanafunzi wengi tu. Shule hiyo wanafunzi bado wana kaa chini, madarasa mengine yamebomoka, madawati mengine yamevunjika yameachwa bure. “Mkuu wa Wilaya yupo, Mkuu wa Mkoa yupo, Mkurugenzi wa Ubungo bado anakusanya kodi yupo na Mbunge wa Ubunge yupo tena yupo hapa na ni profesa tena wa Elimu, simama profesa (Kitila Mkumbo) wakuone kwenye jimbo lako, anafundisha elimu, mimi napenda kusema uwazi,” ”Tena wanazungukia maeneo hayo, lakini hiyo shule ya Ubungo Barango, wanakaa chini na wanaona, nina mshukuru huyo mwandishi ameitoa kwenye mitandao, viongozi wa kule wakaanza kusema ni masuala ya kisiasa, hayo sio masuala ya kisiasa hayo ndiyo ninayopenda kuyajua. “Ninazungumza nikiwa Kagera lakini nikienda Dar Es Salaam niyakute hayo madarasa yamekamilika na wanafunzi hawakai chini, nitaenda kuitembelea hiyo shule kama wananisikia wa Dar es Salaam ujumbe umefika”
habarileo Monday, January 18, 2021 2:53:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
(
about Rais Dk
)
:
“Niwapongeze kwa sherehe za Mapinduzi ya miaka 57, lakini pia nimpongeze Rais Dk Mwinyi ni kiongozi mzuri hata mapato ya Zanzibar yameanza kupaa. Usiogope kutumbua, tumeanza kuona mwanga wa maendeleo na tunaiona Zanzibar ikiwa kama Dubai,”
habarileo Friday, January 15, 2021 9:54:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Maalim Seif amefanya kazi na baba yake Dk Mwinyi yaani Rais wa Awamu ya Pili (Ali Hassan Mwinyi) na leo anafanya kazi na mtoto wake (Dk Hussein Mwinyi), ana uzoefu mkubwa katika uongozi ninaomba mpe ushirikiano sana,”
habarileo Friday, January 15, 2021 9:54:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Ndio, siasa zilivunja hata ndoa, kisa mmoja Mpemba na mwingine Muunguja sababu za kibaguzi tu, lakini baada ya maridhiano ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, leo wote ni wamoja na Rais Dk Hussein anaendelea kuvunja ubaguzi huo, Maalim Seif hakikisha unamsaidia rais wako kurudisha mali za Wazanzibari,”
habarileo Friday, January 15, 2021 9:54:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
"Sisi Watanzania na wakazi wa kanda hii tunaona ni zawadi kubwa kwa wewe (Rais Nyusi) kuja kuweka jiwe la msingikwa sababu nimemleta hapa Rais (Filipe Nyusi) kuweka jiwe la msingi, mmejichongea, hospitali lazima ikamilike, hatuwezi kumleta Rais hapa halafu siku nyingine ananipigia simu vipi ile hospitali niseme bado inajengwa hilo sitakubali."
habarileo Tuesday, January 12, 2021 2:46:00 AM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Pia tumeomba tusamehewe deni la kiwanda cha Urafiki dola milioni 15, tumewaomba kwa sababu China ni marafiki wetu na nchi tajiri. Tunajua kwa sheria za China kutoa msamaha ni ngumu lakini tumeoma ili waangalie namna ya kutusaidia,”
mtanzania Sunday, January 10, 2021 9:37:00 AM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Nimeomba watusaidie katika miradi mikubwa mitatu, ule wa Hydroelectricity power wa Njombe Rumakali na Luhuji, nimeomba watujengee barabara kuu ya kilometa 148 kule Zanzibar, lakini pia nimeomba watufutia madeni yetu likiwemo lile tulilolibeba wakati tunajenga reli ya TAZARA la dola milioni 15.7,”
habarileo Friday, January 8, 2021 3:08:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Watufutie tu kwa sababu nchi ya China ni rafiki yetu na ni nchi tajiri, Mheshimiwa waziri amesema atalifikisha hili ombi,”
habarileo Friday, January 8, 2021 3:08:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kwa ujumla mazungumzo tuliyoyafanya yalikuwa mazuri na nimemhakikishia Tanzania itaendelea kushirikiana na China kwa sababu ni ndugu zetu, sasa ni wakati wa Tanzania na China kujenga uchumi kwa nguvu zote na kuonesha ushirikiano mkubwa,”
habarileo Friday, January 8, 2021 3:08:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Tumeona vyama vingi havina itikadi hivyo kuanizishwa kwa chuo hichi ni mkombozi kwa wananchi kwani watapata viongozi ambao watakuwa wameandaliwa kwa kuwa na maadili mema,”
habarileo Friday, January 8, 2021 11:15:00 AM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Kuuli siyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga kuanzia sasahivi,”
mtanzania Monday, December 28, 2020 1:36:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Maelfu ya watu wanaendelea kupoteza maisha kila siku, lakini Tanzania imeepushwa na janga hilo na maisha ya Watanzania yanaendelea kama kawaida,”
habarileo Saturday, December 26, 2020 6:12:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
(
about Harold Nsekela
)
:
“Nilimweleza Jaji Harold Nsekela na tulikubaliana kwamba mnaweza kuzipakua fomu kutoka kwenye mtandao, lakini ukishazijaza usizirudishe kwa njia ya mtandao, kila mmoja anajua anarudisha fomu yake wapi kulingana na nafasi yake ya kazi, nafahamu kwa mfano Mheshimiwa Spika huwa analeta kwangu, wewe (Mwangesi) unaleta kwangu, mimi nazileta kwako,”
habarileo Friday, December 25, 2020 1:31:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Nachukua nafasi hii kumpongeza Dk Hussein Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuapa kuwa Mjumbe wa baraza hili la mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nakupongeza sana na karibu kwenye kikao chetu,”
habarileo Thursday, December 17, 2020 9:13:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Haya ndiyo maswali magumu mnayotakiwa kuyafanya, yale mliyoyasoma kwenye nadharia myaweke kwenye vitendo na kuona ni kitu gani kimeshindikana kuwapatia maeneo ya kuchimba madini ya chuma wenye viwanda vya kutengeneza nondo na chuma ili wachimbe, hata kama ni kwa kuwapa bure kwa sababu atatengeneza ajira kwa watu watakaochimba chuma, kwenye sekta ya usafirishaji, ajira viwandani na serikali itakusanya mapato,”
habarileo Saturday, December 12, 2020 10:18:00 AM EAT
Rais Magufuli alisisitiza
:
“Tumesikia Kiwanda Cha Saruji Dangote kule Mtwara, akienda kule anapimiwa, na nimeambiwa kuna mtu amehodhi pale, sifahamu kama keshaondoka au bado yupo? Kwa nini hii coal ya Tanzania isitumike kama nishati mbadala wakati wataalamu wapo? Sasa ni jukumu la ninyi Wizara ya Madini kujipanga. Mfanye kazi vizuri usiku na mchana ili zawadi ya madini mengi tuliyopewa na Mwenyezi Mungu yaanze kutumika,”
habarileo Saturday, December 12, 2020 10:18:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Tumeona tukuweke wewe ukawe kiungo kizuri kwenye wizara hii, wewe ni Profesa lakini haina maana kwamba maprofesa waliowahi kukaa kwenye Wizara ya Madini walifanya vizuri. Kwa hiyo nenda na mtazamo huu, kwa sababu tuliwahi kuwa na waziri na katibu mkuu maprofesa, tena wa madini, lakini mambo hayakwenda vizuri,”
habarileo Saturday, December 12, 2020 10:18:00 AM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Ni vizuri ukafanye uamuzi mbaya kuliko kutokufanya uamuzi, unashindwa kutoa uamuzi kwasababu hutaki uonekane mbaya, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita miradi ya maji zaidi ya 1,400 imekamilika, kwa hiyo mkafanye kazi, kafanyeni uamuzi hasa unaohusu maslahi ya taifa”
mtanzania Thursday, December 10, 2020 1:41:00 PM EAT
Rais Magufuli amesisitiza
:
“Ndani ya Serikali sasa hivi kuna ugonjwa mmoja wa ajabu, kwamba hata mawasiliano yanatumwa kwenye ‘ group za WhatsApp , barua nyingine ni za siri na zinaishia kuvuja. Tuzingatie maadili ya viapo vyetu na tufanye kazi zetu kwa uadilifu mkubwa, Serikali hufanya kazi kwa maandishi”
mtanzania Thursday, December 10, 2020 1:41:00 PM EAT
Rais Magufuli alisisitiza
:
“Nataka wanafunzi wetu wafundishwe historia ya Tanzania na hii itasaidia kujenga uzalendo, vijana hawajui historia ya nchi yetu, inawezekana masomo haya yatasaidia kujua jinsi wageni walivyokuja wakadanganya wazee wetu”
mtanzania Thursday, December 10, 2020 1:41:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
(
about Waziri Mkuu
)
:
"Wote nimewaangalia hata wewe uliyeshindwa kuapa na tutateua mtu mwingine ambaye ataweza kuapa vizuri, najua Waziri Mkuu ananiangalia kwa sababu Lindi wametoka yeye na huyu aliyeshindwa kuapa, sasa tutamteua mwingine na wewe tutacheki digrii yako vizuri"
bbc-swahili Thursday, December 10, 2020 7:16:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
"Najua katika kipindi cha miaka mitano mpaka leo, nilitakiwa niwe nimewanyonga watu 256 waliohukumiwa kunyongwa, lakini sijamnyonga hata mmoja,"
habarileo Thursday, December 10, 2020 6:59:00 AM EAT
Rais Magufuli alihoji
:
"Kwa hiyo nimeshindwa kuwaua. Mnisamehe kwa hilo kwa sababu mimi ndio nitakuwa muuaji wa kuuwa wengi kwa sababu wenzangu wameua mtu mmoja au wawili au watatu na wakahukumiwa kunyongwa, halafu mimi niue 256. Si nafuu mimi ninyongwe hapo hapo hata bila kupelekwa mahakamani?,"
habarileo Thursday, December 10, 2020 6:59:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Ndani ya Serikali sasa hivi kuna ugonjwa mmoja, kwa sababu hata mawasiliano yanatumwa kwenye ‘ma-group’ wakati barua zingine ni za siri, mtu anasema tunatakiwa tukutane mahali fulani saa fulani na ajenda yetu ni hii na hii, unakuta labda Makatibu Tawala wa Wilaya wanaandikiana hivyo au Wakuu wa Wilaya au Mawaziri au Makatibu Wakuu na ndiyo maana siri ndani ya serikali zinavuja,”
habarileo Thursday, December 10, 2020 4:45:00 AM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“WAFUNGWA 256 waliohukumiwa kunyongwa wamepunguziwa adhabu na sasa watafungwa Maisha, Sitaki kutenda dhambi,”
habarileo Wednesday, December 9, 2020 3:35:00 PM EAT
Rais Magufuli Alisema
:
"Wote walikuwa wanafaa kupewa uwaziri au unaibu uwaziri. Ilikuwa kazi nzito kufanya uamuzi, Kuna vitu vingi ambavyo tumeviangalia katika uteuzi tuliofanya."
bbc-swahili Wednesday, December 9, 2020 1:21:00 PM EAT
Rais Magufuli anasema
:
“Nitumie fursa hii kulipongeza Bunge la 11 kwa kutoa mchango mkubwa katika kupatikana kwa mafanikio haya,”
habarileo Tuesday, December 8, 2020 8:34:00 AM EAT
Rais Magufuli anasema
:
“Pia serokali itawawezesha wachimbaji wetu wadogo, ikiwa ni pamoja na kuwatengea maeneo ya uchimbaji, kuwapatia mafunzo, mikopo pamoja na vifaa. Na natambua kuwa, wapo baadhi ya watu wamepewa leseni za utafiti na uchimbaji lakini hawajazifanyia kazi; tutazifuta leseni zao, na maeneo hayo kuyagawa kwa wachimbaji wengine, hususan wachimbaji wadogo. Wachimbaji wadogo ni muhimu sana katika kukuza sekta ya madini,”
habarileo Tuesday, December 8, 2020 8:34:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
(
about Harold Nsekela
)
:
“Jaji mstaafu Nsekela alikuwa mwadilifu, mzalendo, asiyejikweza na mchapa kazi. Mungu amweke mahali pema Amina,”
mtanzania Monday, December 7, 2020 7:11:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Nchi yetu pia imebarikiwa kuwa na maeneo mengi yanayofaa kwa shughuli za uvuvi, ikiwemo Ukanda wa Pwani, maziwa, mito na mabwawa. Hali hii inafanya sekta hii kuwa na nafasi ya kutoa mchango mkubwa kwenye kukuza Pato la Taifa na pia kupambana na umasikini na tatizo la ajira. Hata hivyo, kwa sasa, mchango wake bado ni mdogo,”
habarileo Tuesday, December 1, 2020 4:55:00 PM EAT
Rais Magufuli alieleza
:
“Hata hivyo, mapato yaliyokuwa yamekusanywa kwa kipindi cha miaka tisa (2009 hadi 2017) yalikuwa shilingi bilioni 29.79, sawa na shilingi bilioni 3.3 kwa mwaka. Kiwango hiki cha mapato hakikubaliki. Hii ndiyo sababu, tunataka, kwenye miaka mitano ijayo, kusimamia vizuri shughuli za uvuvi wa bahari kuu ili Taifa letu linufaike na rasilimali zake, kwa kuhusisha sekta binafsi. Kwa bahati nzuri, tayari, mwaka huu (2020) tumetunga Sheria Mpya ya Kusimamia na Kuendeleza ya Uvuvi wa Bahari Kuu,”
habarileo Tuesday, December 1, 2020 4:55:00 PM EAT
Rais Magufuli alieleza
:
“Tunakusudia pia kujenga bandari kubwa ya uvuvi itakayotoa ajira zipatazo 30,000; na tutaendelea kuihamasisha sekta binafsi kujenga viwanda vya kuchakata samaki,”
habarileo Tuesday, December 1, 2020 4:55:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
"Lengo la serikali ni kuendelea kuboresha elimu inayotolewa ili iweze kutoa maarifa na ujuzi wa kutosha kwa wahitimu, tutahimiza ufundishaji wa masomo ya sayansi na hisabati hususan kwa wanafunzi wa kike”. “Tunakusudia kujenga shule moja ya sekondari kwenye kila mkoa kwa ajili ya kufundisha masomo ya sayansi kwa wasichana,"
habarileo Thursday, November 26, 2020 1:34:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kwenye miaka mitano ijayo pia, tumejipanga kuendeleza jitihada za kukuza uchumi. Kama unavyofahamu, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, tulijitahidi kusimamia vizuri uchumi wetu, ambapo ulikua kwa wastani wa asilimia saba kwa mwaka,”
habarileo Wednesday, November 18, 2020 11:54:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Aidha, tulifanikiwa kupunguza umasikini wa kipato hadi kufikia asilimia 26.4 kwa takwimu za mwaka 2017/2018. Mafanikio haya, bila shaka, ndiyo yamewezesha, mwezi Julai 2020, nchi yetu kutangazwa kuingia kundi la nchi za uchumi wa kati kutoka kundi la nchi masikini. Na mafanikio hayo yamepatikana miaka mitano kabla ya muda uliopangwa, yaani mwaka 2025,”
habarileo Wednesday, November 18, 2020 11:54:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Na katika hilo, tunalenga kukuza uchumi wetu kwa wastani wa angalau asilimia 8 kwa mwaka na pia kutengeneza ajira mpya zipatazo milioni nane. Tutaendelea pia kuboresha sera zetu za uchumi jumla na sera za fedha na pia kuhakikisha viashiria vyote vya uchumi; ikiwemo thamani ya sarafu yetu, mfumuko wa bei pamoja na viwango vya riba; vinabaki kwenye hali ya utulivu,”
habarileo Wednesday, November 18, 2020 11:54:00 AM EAT
Rais Magufuli amehoji
:
“Na mimi ningeomba wabunge presha mzishushe sababu kazi tuliyoomba hapa ni ubunge wala siyo uwaziri, tulitoka hapa wengine mlikuwa wabunge kwenda kuomba ubunge kwamba tutawatumikia wananchi wetu na tukakabidhiwa ilani ya uchaguzi yenye kurasa 303 sasa mengine yanatoka wapi?,”
mtanzania Monday, November 16, 2020 3:06:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Hivyo kuna vigezo vingi na kazi ni ngumu kwa hiyo lazima uwe na usawa na umtangulize Mungu ili anayestahili usije ukamuonea. Kwa hiyo ninawaomba tu ndugu zangu mnisamehe tu kwamba inachukua muda mrefu,”
mtanzania Monday, November 16, 2020 3:06:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
(
about Palamagamba Kabudi
)
:
“Kwenye Wizara ya Mambo ya Nje napo hatuwezi tukakosa mtu wa kutusemea tukaendelea kutukanwa watu wanatengeneza majambo yao hawapati majibu kwa sabubu nchi yetu haiwezi kujifungia nikaona Prof. Kabudi naye alimudu nafasi yake nikaona nimrudishe,”
mtanzania Monday, November 16, 2020 3:06:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Hivyo ni suala ambalo halihitaji haraka, kwa hiyo nawaomba sana wabunge najua maneno ni mengi, kwa kwa waganga nendeni shauli yenu, wengine watawapaka mikosi lakini najua hamuendi,”
mtanzania Monday, November 16, 2020 3:06:00 PM EAT
Rais Magufuli Alisema
:
''Si kwamba hawa wawili ni maarufu sana kuliko waliobaki, miaka ya nyuma niliwateua hawakuwa na majimbo, na niliwaambia waende kwenye majimbo au waende huko walikotoka, wakaenda kwenye majimbo.''
bbc-swahili Monday, November 16, 2020 2:41:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kwa msingi huo napenda nirudie kupongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kusimamia vizuri uchaguzi mkuu mwaka huu; kuanzia uandikishaji wapigakura, uchukuaji na urejeshaji fomu za wagombea, usimamizi wa kampeni, upigaji kura na utoaji wa matokeo mapema,”
mwananchi Sunday, November 15, 2020 10:49:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Na katika hilo, naahidi kushirikiana kwa karibu sana na Rais mpya wa Zanzibar, Mheshimiwa Dk Hussein Mwinyi. Kamwe, hatutakuwa na mzaha na yeyote mwenye kutaka kuhatarisha amani ya nchi yetu; mwenye nia ya kuvuruga umoja na mshikamano wetu; na pia mwenye kutaka kutishia Uhuru wetu, Muungano na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,”
habarileo Saturday, November 14, 2020 11:12:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Hatutaki mtu yeyote anayetaka kuwekeza asumbuliwe na masuala yasiyo na msingi. Tunahitaji kuwa na mabilionea wengi wa Kitanzania wakiwemo wabunge. Tunataka Watanzania wote washiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi yao,”
habarileo Saturday, November 14, 2020 11:12:00 AM EAT
Rais Magufuli alisisitiza
:
“Namuahidi Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwenye miaka mitano ijayo serikali itatoa ushirikiano mkubwa na kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Zanzibar. Tutafanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kuleta maendeleo kwa pande zote za Muungano,”
habarileo Saturday, November 14, 2020 11:12:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kumekuwepo na vikwazo vingi kwa wawekezaji ikiwemo urasimu mwingi, wawekezaji kuzungushwa na kukatishwa tamaa, nataka mwekezaji mwenye fedha zake akija apate kibali ndani ya siku 14,”
habarileo Saturday, November 14, 2020 11:12:00 AM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Sambamba na hayo, kuhusu nishati, kwenye miaka mitano ijayo, tutaanza utekelezaji wa Miradi ya kielelezo (flagship projects) ya Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga lenye urefu wa kilometa 1,445 pamoja na Mradi wa Kusindika Gesi Asilia (LNG) Mkoani Lindi,”
mtanzania Friday, November 13, 2020 6:34:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Zaidi ya hapo, tutaendelea kuhamasisha matumizi ya gesi asilia na gesi ya mitungi majumbani, kwenye taasisi, viwanda na magari ili kupunguza uharibifu wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi,”
mtanzania Friday, November 13, 2020 6:34:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Jambo la kwanza na muhimu tutakalolipa kipau mbele kikubwa kwenye miaka mitano ijayo ni kuendelea kulinda na kudumisha tunu za taifa letu yaani amani, umoja na mshikamano, uhuru wa nchi yetu, muungano na mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Na katika hilo naahidi kushirikiana kwa karibu sana na Rais mpya wa Zanzibar mheshimiwa Dr. Hussein Mwinyi, kamwe hatutakuwa na mzaha na yoyote mwenye kutaka kuhatarisha amani ya nchi yetu”
deutschewelle-sw Friday, November 13, 2020 2:27:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Hakuna demokrasia isiyo na mipaka, aidha uhuru na haki vinakwenda sambamba na wajibu na hakuna uhuru au haki isiyokuwa na wajibu. Vyote vinakwenda sambamba. Najua nimeelewaka vizuri. Mheshimiwa spika, kama nilivyoahidi wakati wa kipindi cha kampeini kwenye miaka mitano ijayo tutaendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa wajasiriamali wadogo”
deutschewelle-sw Friday, November 13, 2020 2:27:00 PM EAT
Rais Magufuli aliandika
:
“Kwa niaba ya serikali na Watanzania, nakupongeza Rais Mteule wa Marekani Joe Biden pamoja na Makamu wa Rais, Kamala Harris kutokana na ushindi wenu katika Uchaguzi Mkuu wa Marekani. Nakuhakikishia kuwa Tanzania italinda na kuendeleza uhusiano uliopo baina ya nchi zetu,”
habarileo Thursday, November 12, 2020 11:14:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Hivyo ninaomba waheshimiwa wabunge na Watanzania wote mniombee na mniunge mkono wakati natumbua majipu haya,”
habarileo Thursday, November 12, 2020 9:24:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kero hizi tutazishughulikia kwa nguvu zetu zote. Wizara, ofisi na taasisi husika zijipange ipasavyo kutatua kero hizi. Nimetaja baadhi ya kero hizi ili nanyi waheshimiwa wabunge mzitambue na mshirikiane na serikali na wadau wengine tuzitatue haraka,”
habarileo Thursday, November 12, 2020 9:24:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kwa kweli tangu nimefika hapa Tanzania nimeona mambo mazuri na ambayo tunapaswa kuyaiga sisi viongozi wa mataifa mengine,”
habarileo Wednesday, November 11, 2020 9:13:00 AM EAT
Rais Magufuli alihoji
:
“Nilitaka nichomekee hapa, kumekuwa na tabia kila serikali mpya au awamu nyingine inapoingia watu wanakuwa na hofu hasa watendaji ndani ya serikali kwamba kunatokea mabadiliko. Sasa wakuu wa mikoa na wilaya wana hofu sana, nawashangaa kwa nini wanakuwa na hofu,”
habarileo Tuesday, November 10, 2020 8:44:00 AM EAT
Rais Magufuli alifafanua
:
“Wanasiasa ambao tumeguswa na hili, mimi rais na makamu wangu, waziri mkuu na mawaziri, mwingine atakayeguswa ni spika na naibu ambao sisi tunapigiwa kura. Sasa mkuu wa mkoa unakuwa na wasiwasi gani ‘unless performance’ yako haikuwa nzuri. Napata meseji kuwa mkuu wa mkoa anasema nimefanya vizuri kwenye kipindi chako,”
habarileo Tuesday, November 10, 2020 8:44:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Kuapisha kunachosha, uanze kuapisha wakuu wa mikoa 26, Ras 26, siwezi. Nitaapisha yule atakayejiondoa mwenyewe. Mchape kazi msiwe na wasiwasi. Tukatatue shida za wananchi”
habarileo Tuesday, November 10, 2020 8:44:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Katika kipindi chako cha mwanzo ulijitahidi kufanya kazi vizuri, ndio maana tumekupa tena hii nafasi ili ukafanye vizuri zaidi, kikubwa ukamtangulize Mungu katika majukumu yako, maana mimi naamini uwezo unao, Mungu yupo, nina uhakika utafanya makubwa zaidi,”
habarileo Tuesday, November 10, 2020 8:44:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Mwigulu ninamfahamu...na Profesa Mkumbo naye nampenda, ndiyo maana nikasema huyu agombee hapa na yule akagombee Ubungo na nataka wote washinde,”
mwananchi Monday, November 9, 2020 6:43:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
(
about Rais Magufuli
)
:
“Mkuu wa mkoa unakuwa na wasiwasi gani, labda kama utendaji wako haukuwa vizuri, kwa sababu nashangaa napata vimeseji vingine, ‘mheshimiwa, Rais nimejitahidi katika kipindi changu’ kana kwamba nilimwambia kipindi chake kinaisha baada ya mimi kuapishwa,”
mwananchi Monday, November 9, 2020 5:08:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Mabadiliko yatakayokuwepo ni kwenye mawaziri, kuna ambao watarudi na kuna ambao hawatarudi hili sitaki kusema uongo, nikishamaliza hilo basi wengine wachape kazi tu,”
mwananchi Monday, November 9, 2020 5:08:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Mkuu wa mkoa unakuwa na wasiwasi gani labda kama ulikuwa ufanyi kazi vizuri kwasababu nashangaa napata vimesji vingine Mhe Rais nimejitahidi katika kipindi changu kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa nimeona hili nilizungumze kwamba Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya msiwe na wasiwasi”
mtanzania Monday, November 9, 2020 1:24:00 PM EAT
Rais Magufuli Amesema
:
“kwanini nibadilishe Mkuu wa mkoa, kwanini nibadilishe mkuu wa Wilaya, kwanini nibadilishe Mkurugenzi, kwanini nibadilishe DAS Serikali ni ile ile”
mtanzania Monday, November 9, 2020 1:24:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
"Kama tulivyoanza kuchangia kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa kanisa hili, nakuomba sana kama utaniruhusu Askofu na kama sitakukwaza tuchange angalau tuanze kujenga msikiti wa ndugu zetu Waislamu."
habarileo Monday, November 9, 2020 8:01:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
(
about Kassim Majaliwa
)
:
“Hata kufanya kazi na mimi ni kazi ngumu, lazima ujipange sawasawa, na hili nawaeleza ukweli kwa sababu na mimi ni mgumu. Hili Majaliwa ameliweza,”
mwananchi Saturday, November 7, 2020 4:02:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Jukumu kubwa na muhimu lililopo mbele yetu hivi sasa ni kuendeleza jitihada za kulijenga na kuleta maendeleo kwa taifa letu. Na katika hilo niwahakikishie Watanzania wenzangu kuwa kiapo nilichokiapa hivi punde na alichoapa Makamu (Samia Suluu Hassan) tutahakikisha tunakienzi kwa nguvu zote,”
habarileo Friday, November 6, 2020 6:26:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Uwepo wenu hapa na salama mlizotutumia, sio tu zinatupa nguvu za kuwatumikia wananchi vizuri, bali ni ishara ya uhusiano na ushirikiano uliopo kati yetu. Napenda niwahahakishie kama ilivyokuwa kwenye miaka mitano iliyopita, kwenye miaka mitano ijayo tutaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano kati yetu pamoja na taasisi mnazoziwakilisha,”
habarileo Friday, November 6, 2020 6:26:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Hii ni ishara nyingine kuwa Mungu analipenda taifa letu la Tanzania, tangu tumepata Uhuru mwaka 1961, nchi imepita kwenye mitihani mingi na Mungu ametuvusha salama...Tumshukuru sana Mungu kwa maajabu anayolifanyia taifa hili,”
habarileo Friday, November 6, 2020 6:26:00 AM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Hata njaa kali ilipoingia nchini mwetu, Tanzania walitupatia mahindi, hata Uganda nao walituletea mahindi, ndio viongozi wazalendo kabisa katika ukanda wetu,”
habarileo Thursday, November 5, 2020 4:13:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Sambamba na hilo tutatekeleza kwa namna kubwa katika kukuza uchumi na kushughulikia changamoto za umasikini zinazowakabili Watanzania. Ukosefu wa ajira kwa vijana na kero mbalimbali kwa wananchi,”
habarileo Thursday, November 5, 2020 2:28:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Uchaguzi umekwisha, uchaguzi umekwisha, uchaguzi umekwisha. "Uchaguzi sasa umekwisha, jukumu kubwa lililopo mbele yetu ni kuendeleza jitihada za kujenga na kuleta maendeleo kwa Taifa letu na niwahakikishie kuwa kiapo nilichoapa na alichoapa makamu wangu (Samia Suluhu Hassan), tutahakikisha tunakienzi kwa nguvu zote,”
habarileo Thursday, November 5, 2020 2:28:00 PM EAT
Rais Magufuli alieleza
:
“Gharama ya umeme wetu ipo juu na uwezo wetu wa kuzalisha kwa sasa ni megawati 1,600, mradi huu wa megawati 2,115 ukikamilika tutausambaza umeme nchi nzima na tutaushusha bei kwa sababu huwezi kujenga uchumi wa viwanda kama huna umeme wa uhakika na wa gharama nafuu, mpaka sasa viwanda vipya 8,470 vimeanzishwa maeneo mbali mbali hapa nchini,”
habarileo Thursday, November 5, 2020 9:04:00 AM EAT
Rais Magufuli alieleza
(
about Tanzania Bara
)
:
“Mwaka 2012, Benki ya Dunia ilisema Tanzania itaweza kufikisha umeme kwenye vijiji vyote 12,280 ifikapo mwaka 2100, mimi nasema tutapeleka umeme kwenye vijiji vyote ndani ya miaka mitano ijayo,”
habarileo Thursday, November 5, 2020 9:04:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Baba wa Taifa alikuwa haongozwi ongozwi wala kupelekeshwapelekeswa. Tukasema haiwezekani Watanzania ambao chakula chao chenyewe wanakitafuta kila siku, leo ufungiwe nyumbani,”
habarileo Thursday, November 5, 2020 7:32:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Tutaimarisha masoko kwenye maeneo yenye shughuli za uchimbaji madini na kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya uchenjuaji madini,”
habarileo Thursday, November 5, 2020 5:14:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Nitaimarisha pia Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kiwe na uwezo wa kutoa wataalamu mbalimbali wa anga. Lakini pia nitaongeza matumizi ya intaneti kutoka asilimia 43 ya sasa hadi kufikia asilimia 80,”
habarileo Thursday, November 5, 2020 5:14:00 AM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Serikali nitakayoiunda itakuwa ya uwazi, uwajibikaji na usawa bila kubagua mtu kwa rangi au eneo analotoka ambayo itakayokuwa ikizingatia nidhamu kwa watumishi, itakayokuwa na kasi kwa kuimarisha huduma za kijamii.”
habarileo Monday, November 2, 2020 3:48:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
(
about Rais Magufuli
)
:
“Nasimama mbele yenu kwa mara ya kwanza nikiwa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Nimekula kiapo kuwa Rais wa nane wa Zanzibar,”
habarileo Monday, November 2, 2020 3:48:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Mmetupa ushindi mkubwa sana ambao umetuachia deni kubwa sana, ninamuomba Mungu anisaidie katika kipindi hiki cha pili tuweze kukidhi haja za Watanzania,”
mwananchi Sunday, November 1, 2020 1:58:00 PM EAT
Rais Magufuli aliongeza
:
“zimebakia siku moja ili Watanzania mkapige kura kwa kuamua mazuri, hivyo ni vizuri kuitumia siku hiyo katika kujenga umoja wa watanzania”
habarileo Tuesday, October 27, 2020 2:23:00 AM EAT
Rais Magufuli alisema
(
about Waziri Mkuu
)
:
“Ndani ya mwezi mmoja muwe tayari kutatua tatizo hilo, kama hakuna fedha kama ambavyo meneja amesema zungumza na Waziri wa Fedha au Katibu Mkuu ili kushughulikia suala hilo,”
habarileo Monday, October 26, 2020 7:28:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Nilienda Rwanda nilialikwa na Rais Paul Kagame, akaenda kunitembeza kwenye jumba la makumbusho ya mauji ya Kimbari. Nilienda kujifunza umuhimu wa kutunza amani, yaani niliona mafuvu ya vichwa vya watu maelfu mpaka Watoto. Ukiona unachanganyikiwa,”
habarileo Sunday, October 25, 2020 8:22:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Nimesikitishwa na vifo vya watanzania wenzetu waliopoteza maisha katika ajali hii, nawapa pole wafiwa wote na nawaomba wawe na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi kigumu cha majozi,”
habarileo Sunday, October 25, 2020 6:51:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Na huu ni ukweli na siwezi kuuficha, na hili liwe fundisho kwetu sisi Watanzania na vizazi vinavyokuja baadaye, kwamba kubinafsisha ndege, treni na meli ni dhambi kubwa,”
habarileo Sunday, October 25, 2020 6:51:00 PM EAT
Rais Magufuli alisema
:
“Lakini pia hivi karibuni mtaanza ujenzi wa reli ya Katavi kwenda Bandari ya Kalema ili kurahisisha usafiri kati yetu na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),”
habarileo Sunday, October 25, 2020 6:51:00 PM EAT
Rais Magufuli amesema
:
“Niwahimize Watanzania wenzangu tupende vya kwetu na nitashangaa sana kama vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vitaendelea kuagiza viatu kutoka nje nitashngaa sana wanafunzi waendelee kuvaa viatu vya nje,”
mwananchi Thursday, October 22, 2020 4:40:00 PM EAT